Air Zimbabwe yapigwa marufuku kuruka katika anga ya Ulaya
Umoja wa Ulaya umetangaza uamuzi wa kupiga marufuku shirika la ndege la Air Zimbabwe kuruka kwenye anga yake kutokana na sababu za kiusalama.
Jumatatu wiki hii, Kamati ya Ulaya ilitangaza orodha mpya kuhusu usalama wa anga, ambayo inapiga marufuku mashirika 181 ya ndege ya nchi 16 yasiyo ya Ulaya, yasiyotimiza vigezo vya usalama vya kimataifa kuruka kwenye anga yake.
Nchi nyingine za Afrika zilizoathiriwa ni pamoja na Angola, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Eritrea, Guinea ya Ikweta, Gabon, Liberia, Sierra Leone, Nigeria na Sudan.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |