• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (3 Juni-9 Juni)

    (GMT+08:00) 2017-06-09 19:13:25
    Mataifa sita yavunja uhusiano na Qatar

    Mataifa sita ya Kiarabu, zikiwemo Saudi Arabia, Misri, Bahrain, Umoja wa Milki za Kiarabu na Yemen, yamekata uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar yakiilaumu kwa kuvuruga uthabiti katika eneo hilo.

    Nchi hizo zimeilaumu Qatar kwa kuunga mkono makundi ya kigaidi, likiwemo kundi la Islamic State (IS).

    Shirika moja nchini Saudi Arabia linasema kuwa taifa hilo limefunga mipaka yake na kusitisha usafiri wa ardhini, baharini na angani.

    Qatar hata hivyo imeapa kwamba haitasalimu amri katika mzozo wake kuhusu sera yake ya kigeni na nchi nyingine za Kiarabu huku shirika la habari la Al Jazeera likivamiwa na wadukuzi.

    Waziri wa mambo ya nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al-Thani amesema anaunga mkono zaidi kutumiwa kwa demokrasia kutatua mzozo huo na kwamba hakuwezi kuwa na suluhu inayoweza kupatikana kupitia nguvu za kijeshi, ameambia Reuters.

    Qatar imepuuzilia mbali tuhuma hizo kwamba inaunga mkono makundi ya Kiislamu yenye msimamo mkali.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako