Rais wa Togo achaguliwa kuongoza ECOWAS
Rais wa Togo Faure Gnassingbé ndiye rais wa sasa wa jumuiya ya kiuchumi ya nchi Afrika Magharibi ECOWAS.
Alichaguliwa siku ya Jumapili Juni 4 katika mkutano wa 51 wa viongozi wa nchi wanachama wa ECOWAS mjini Monrovia, nchini Liberia.
Anachukuwa nafasi ya rais wa Liberia Ellen Johanson Sirleaf
Faure NGnassingbe alitoa wito kwa ushirikiano zaidi na kupongeza maendeleo ya kiuchumi yaliofikiwa katika ukanda huo wa Afrika Magharibi, wakati ambapo moja ya maamuzi ya mkutano huo ni kujenga barabara kuu kati ya Abidjan na Dakar.
Mfalme wa Morocco Mohammed VI hakuhudhuria mkutano huo, baada ya kufuta ziara yake katika dakika za mwisho, kwa sababu ya kuwepo kwa mgeni mwingine maalum amabye ni Waziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu.
Niger iliwakilishwa katika mkutano wa Monrovia na balozi wake huku duru zikiarifu kuwa wa nchi hiyo Mahamadou Issoufou amekataa mwaliko kutokana na kuwepo kwa Waziri Mkuu wa Israel. Niger haina uhusiano wa kidiplomasia na Israel kwa miaka kadhaa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |