Raia 31 wa China wanaoshikiliwa nchini Zambia hawajaachiwa huru
Raia 31 wa China waliokamatwa hivi karibuni na idara ya uhamiaji ya Zambia kwa madai ya kununua madini ghafi ya shaba kinyume na sheria bado hawajaachiwa huru.
Balozi wa China nchini Zambia Bw. Yang Youming alikutana na waziri wa mambo ya ndani wa Zambia Bw. Stephen Kmapyongo, ambapo balozi Yang amesema China inaitaka Zambia ishughulikie kesi hiyo kwa mujibu wa sheria na kuwaachia huru raia hao.
Baadaye wiki hii Rais Edgar Lungu wa Zambia jana huko Lusaka amekutana na mjumbe wa taifa wa China Bw. Wang Yong ambaye yuko ziarani nchini humo.
Katika mazungumzo yao, Rais Lungu ameeleza imani kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi yake na China, na kusema Zambia inapenda kushirikiana na China kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Kwa upande wake, Bw. Wang Yong amewasilisha salamu za rais Xi Jinping wa China kwa rais Lungu, na kusema China inapenda kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwenye ujenzi wa miundo mbinu, kilimo, raslimali ya watu wenye ujuzi, na viwanda.
Katika ziara yake, Bw. Wang Yong pamoja na rais Lungu wameshuhudia kusainiwa kwa nyaraka za ushirikiano kati ya serikali za nchi hizo mbili, na kukagua baadhi ya kampuni za China nchini Zambia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |