Rais wa Marekani asema uhusiano wa nchi hiyo na Urusi uko hatarini
Rais wa Marekani Donald Trump anasema kuwa uhusiano kati ya nchi yake na Urusi uko hatarini baada ya bunge la Congress kuiongezea Urusi vikwazo.
Bwana Trump alidhinisha hatua hiyo siku ya Jumatano.
Urusi nayo imesema kuwa vikwazo hivyo vipya ni kama kutangaza vita vya biashara dhidi ya Urusi.
Sheria hiyo inalenga kuiadhibu Urusi kwa madai ya kuingilia uchaguzi wa Marekani mwaka 2016 na vitendo vyake nchini Ukrain.
Trump alikuwa amepinga mswaada huo ambao unizichukulia hatua Iran na Korea Kaskazini, na unamzuia Trump kulegeza vikwazo hivyo bila idhini ya Congress.
Urusi imejibu kwa hasira vikwazo hivyo. Waziri mkuu Dmitry Medvedev alisema kuwa vikwazo vinamaliza matumaini ya kuboresha uhusiano kati ya Urusi na Marekani.
Kupitia ujumbe kwenye mtandao wa Facebook Medvedev aliandika kuwa hatua hizo zilionyesha udhaifu wa Trump.
Wiki iliyopita Urusi ilijibu kwa kuiamrisha Marekani kupunguza wanadiplomasia kwa watu 775.
Hatua hiyo inapunguza kiwango cha fedha ambazo Marekani itawekeza katika miradi ya nishati nchini Urusi na kufanya vigumu kwa kampuni za Marekani kufanya biashara na Urusi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |