Serikali ya Syria na upinzani zasitisha vita Homs
Wizara ya ulinzi ya Russia imetangaza kuwa wajumbe wa Russia na makundi ya upinzani ya Syria wamefikia makubaliano kuhusu kupunguza mapambano mkoani Homs, katikati mwa Syria, na kuamua kusimamisha vita kwenye eneo hilo kuanzia tarehe 3.
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Russia Bw Igor Konashenkov amesema wajumbe wa wizara ya ulinzi ya Russia wamejadiliana na wajumbe wa makundi ya upinzani tarehe 31 mwezi Julai mjini Cairo, na kufikia makubaliano ya kusitisha vita, lakini makubaliano hayo hayahusishi makundi ya IS na al-Nusra Front.
Bw Konashenkov ameongeza kwamba kuanzia leo Russia itaweka vituo viwili vya ukaguzi na vituo vitatu vya uangalizi kwa ajili ya kusimamia usitishaji wa mapambano, na kuhakikisha usafirishaji wa majeruhi na msaada wa dharura bila vizuizi.
Na kwingineko Jeshi la serikali la Syria limesema, operesheni iliyofanywa na jeshi hilo imefanikiwa kupata udhibiti tena wa maeneo mengi ya jimbo la Al-Raqqah kutoka kundi la IS.
Katika operesheni hiyo, jeshi hilo liliwashambulia kwa risasi wapiganaji wengi wa IS na kudhibiti visima vya mafuta. Pia jeshi hilo limefanya shambulizi la anga dhidi ya ngome ya kundi la IS katika jimbo la Homs na kuharibu magari mengi ya kundi hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |