• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (29 Julai-4 Agosti)

    (GMT+08:00) 2017-08-04 20:16:50

    COMESA kutuma ujumbe wa uangalizi kwenye uchaguzi mkuu wa Kenya

    Jumuiya ya soko la pamoja la nchi za Mashariki na kusini mwa Afrika COMESA imetoa taarifa mjini Nairobi ikisema itatuma waangalizi 15 kwenye uchaguzi mkuu wa Kenya unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo.

    Timu ya waangalizi hao itaongozwa na aliyekuwa waziri wa sheria wa Zimbabwe Dk Simbi Mubako. Timu hiyo itashuhudia kazi ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo. Siku chache kabla ya uchaguzi huo, timu hiyo itakutana na wadau muhimu wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na vyama vikubwa vya siasa, idara za usalama, tume ya uchaguzi, jumuiya za kiraia, vyombo vya habari na mahakama kujua wamejiandaa vipi kwa ajili ya uchaguzi huo, na mazingira ya kisiasa kabla ya upigaji kura.

    Mchakato wa kufuatilia maendeleo ya uchaguzi huo utafanyika kwa mujibu wa katiba na sheria za Kenya.

    Ikiwa zimebaki siku tatu kabla ya uchaguzi mkuu wa Kenya, wagombea urais kwenye uchaguzi huo leo wanafanya kampeni za mwisho kuomba kura kwa wananchi.

    Wagombea wawili wakuu kwenye uchaguzi huo ni Rais Uhuru Kenyatta akiongoza chama cha Jubilee na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga akiongoa muungani wa NASA.

    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako