Msukosuko wa kibinadamu wa Mosul Iraq bado kwisha
Mratibu wa maswala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Bibi Lisa Grande wiki hii anasema hali ya kibinadamu nchini Iraq inaendelea kuwa mbaya, wakati serikali ikiendelea na kazi ya kuwahamisha watu kabla ya hatua za mwisho kuliondoa kundi la IS.
Bibi Grande amesema licha ya kuwa Syria inabaki kuwa na operesheni kubwa zaidi za mambo ya kibinadamu, watu wengine nchini Iraq wanapoteza makazi yao kwa kasi zaidi kuliko sehemu yoyote duniani.
Ametolea mfano wa Mji wa Mosul ambao amesema licha ya kuondolewa kwa kundi la IS msukosuko wa kibinadamu bado unaendelea, na watu zaidi wanatarajiwa kupoteza makazi yao, baada ya kuanza kwa operesheni nyingine dhidi ya wapiganaji wa kundi la IS katika mji wa Tal Afar karibu na Mosul.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |