Mamia ya raia wakimbia mapigano Saudia
Eneo la Mashari ya Saudi Arabia linaendelea kukumbwa na mapigano kati ya jeshi la nchi hiyo na watu wenye silaha. Maafisa kadhaa wa polisi na watu waliojihami wameuawa katika mpigano ya hivi karibuni.
Mamia ya wakazi wa eneo hilo wamelazimika kuyatoroka makazi yao kutokana na mapigano yaliyoanza tangu wiuki kadhaa zilizopita.
Vikosi vya usalama vimelenga maeneo ya kale ya Awamiya, ambayo wanasema ni sehemu wanakojificha wapiganaji wa Shia.
Maafisa wa utawala wanataka kulibomoa eneo hilo la kale lenye miaka 200 katika operesheni ilioanzishwa mnamo mwezi Mei.
Mji wa Awamiya ni nyumbani anakotoka Sheikh Nimr al-Nimr, kiongozi wa kidini mwenye ushawishi anayewaunga mkono waandamanaji wa Kishia, ambaye aliuawa mwaka mmoja na nusu uliopita.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |