Polisi DRC waonyesha wafuasi wa Bundu wanaotuhumiwa mauaji
Siku ya Jumatano, Agosti 9, mjini Kishasa, polisi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilionyesha wafuasi thelathini wa kundi la Bundu dia Kongo wanaoshtumiwa kuendesha mashambulizi siku ya Jumatatu katika mji mkuu wa nchi hiyo.
Wanawake watatu ni miongoni mwa watuhumiwa hao. Kwa mujibu wa msemaji wa polisi, washambuliaji walikua na nia ya kutoatangazo kwenye runinga ya taifa.
Watuhumiwa hao walisafirishwa na gari la polisi hadi kwenye makao makuu ya polisi, huku wakishindikizwa na kikosi kikubwa cha askari waliojihami kwa silaha za kivita. Wengi wao walikua walivaa vitambaa vyekundu kichwani. Na wengine walikua na beji zenye nembo ya kundi la bundu dia Kongo (BDK). Wote walikua miguu peku, huku nyele zao zikwa hivyo.
Msemaji wa polisi Kanali Ezéchiel Pierrot Rombaut Muanamputu alisema watu hao ni magaidi walioofanya mauaji katika mji mkuu wa DR COngo, Kinshasa siku ya Jumatatu Agosti 7, 2017.
Ameongeza kuwa watu hao ni wafuasi wa Ne Muanda Nsemi, kiongozi wa kiroho wa na kidini wa kundi la Bundu dia Kongo.
Wanawake watatu ambao walionyeshwa katika kundi hilo kama manabii wa kundi la Bundu dia Kongo. Mifuko miwili ya hirizi wa inayodaiwa kuwa ya kundi hilo ilioneshwa.
Vikosi vya usalama viliweza kudhibiti hali ya mabo na kurejesha utulivu kwa muda wa saa zisizozidi mbili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |