• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (4 Septemba-8 Septemba)

    (GMT+08:00) 2017-09-08 21:03:28
    Kimbunga Irma chasababisha maafa Caribbean.

    Kimbunga kilichopewa jina Irma kimeharibu majumba na kusababisha mafuriko makubwa katika visiwa vinavyomilikiwa na Ufaransa katika eneo la Caribbean.

    Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa GĂ©rard Collomb amesema majumba manne imara zaidi katika visiwa vya Saint Martin, ambavyo humilikiwa na Ufaransa na Uholanzi, yameharibiwa.

    Mwishoni mwa wiki kimbunga hicho kimeelekea visiwa vya Turks na Caicos baada ya kusababisha uharibifu mkubwa huko Caribbean na kuwaua takriban watu 14.

    Kumeripotiwa uharibifu na mafuriko nchini Haiti ambapo miundo mbinu bado ni mibaya tangu litokee tetemeo la ardhi mwaka 2010.

    Irma ni kimbunga cha kiwango cha tano.

    Hiki ndicho kiwango cha juu zaidi cha kimbunga na upepo wake una kasi ya kilomita 280 kwa saa.

    Maelfu ya watu wamehamishwa kutoka kwa maeneo yaliyo hatarini.

    Wakazi wamefika madukani kununua chakula, maji na dawa vya kujihifadhia.

    Viwanja vya ndege katika visiwa vingi eneo hilo vimefungwa.

    Katika eneo la Key West katika jimbo la Florida, Marekani, watu wameamrishwa kuhama. Kimbunga hicho kinatarajiwa kufika eneo hilo wikendi.

    Tume ya uchaguzi nchini Kenya yakumbwana malumbano ya ndani

    Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya imetangaza tarehge 17 kuwa siku ya kurejelewa kwa uchaguzi wa Urais baada ya mahakama ya juu nchini humo kufuta matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8.

    Hta hivyo sasa tume hiyo imegumbikwa na malumbano ya ndani huku mwenyekiti wake Wafula Chebukati akimtaka mkurungezi mkuu wake Ezra Chiloba kuelezea bayana kwa nini utambulisho wake wa barua pepe ulitumika kuingia katika seva na kubadilisha matokeo ya kura ya urais.

    Kupitia kwa barua yenye maagizo, Wafula Chebukati anamtaka Chiloba pia kuelezea ni kwa nini fomu za uchaguzi hazikuwa na thibitisho la usalama, ni kwa sababu gani simu zenye kima cha shilingi milioni 848 zinazotumia mtandao wa Satellite zilizonunuliwa na tume hiyo hazikutumika.

    Wakati tarehe ya uchaguzi wa marudio ya kura ya urais ikiendelea kuonekana kuwa kizungumkuti kati ya chama cha Rais Uhuru Kenyatta na Muungano wa Upinzani unaoongozwa na Raila Odinga, bado vuta nikuvute zinaendelea kushuhudiwa nchini Kenya.

    Hata hivyo, Makamishna wa tano wa Tume hiyo ya Uchaguzi wakiongozwa na Naibu Mwenyekiti wa Tume hiyo Consolata Nkatha Maina, Makamishna Yakubu Guliye, Paul Kurgat, Boya Molu na Margaret Mwachanya wamepuuzilia mbali nyaraka barua ya Chebukati kwa Chiloba na kusema kuwa maagizo yaliyonakiliwa hayakuafikiwa katika vikao vya tume hiyo.

    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako