Tetemeko kubwa la ardhi lakumba Mexico.
Tetemeko kubwa la ardhi la nguvu ya 8 katika vipimo vya richa limekumba pwani kusini mwa Mexico.
Kitovu cha tetemeko hilo lilitokea umbalia wa karibu milomita 100 kuisni magharibi mwa mji wa Pijijiapan katika kina cha kilomita 35, kwa mujibu wa idara ya hali ya hewa ya Marekani.
Onyo la kutoea tsumani limetolewa nchini Mexico, Guatemala, El Salvador, Costa Rica, Nicaragua, Panama na Honduras.
Tetemeko hilo lilisikika mji wa wa Mexico City ambapo watu walitoka manyumbani mwao kwenda barabarani.
Mgeni mmoja katika mji huo Luis Carlos Briceno, aliliambia shirika la Reuters, "sijawai kuwa popote pale ambapo ardhi ilisonga sana.
Umeme umeripotiwa kupotea sehemu za mji.
Hakuna onyo la tsunami lililotolewa pwani magharibi mwa Marekani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |