• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (4 Septemba-8 Septemba)

    (GMT+08:00) 2017-09-08 21:03:28

    Tani 1000 za msaada wa kibinadamu zafikishwa Deir ez-Zor, Syria

    Shirika la habari la Syria SANA limeripoti kuwa, magari 40 yaliyobeba misaada ya kibindamu yamewasili mjini Deir ez-Zor baada ya jeshi la serikali kuukomboa mji huo, ulioshikiliwa na kundi la Islamic States IS kwa miaka mitatu.

    Ripoti imesema, msafara huo wa magari ulifika asubuhi kwenye kambi ya kijeshi iliyoko kusini magharibi mwa Deir ez-Zor, ukiwa na tani 1,000 za chakula, dawa, vifaa vya matibabu, vitabu na vifaa vingine vya shule.

    Wakati mji wa Deir ez-Zor uliposhikiliwa na kundi la IS, raia takriban elfu 93 waliokwama mjini humo walikuwa wakikabiliwa na upungufu wa mahitaji, na kuishi kwa kutegemea msaada wa serikali ya Syria na mashirika ya Umoja wa Mataifa, uliopatikana kwa kuangushwa kutoka kwenye ndege.

    Hivi sasa operesheni ya jeshi la serikali ya Syria ya kupambana na kundi la IS bado inaendelea.

    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako