• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (9 Septemba-15 Septemba)

    (GMT+08:00) 2017-09-15 17:46:36

    Japan yalaani kombora la Korea kupitia anga yake

    Korea Kaskazini Ijumaa imefyatua kombora la masafa marefu kupitia anga ya kisiwa cha Hokkaido nchini Japan limesema jeshi la Korea Kusini.

    Jeshi la Korea Kusini linasema kuwa kombora hilo limefyatuliwa kutoka maeneo ya karibu na mji mkuu wa Pyongyang na kupita anga za juu zaidi na kwenda mbali zaidi ikilinganishwa na kombora la awali.

    Jaribio hilo linakuja siku chache tu baada ya baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kuidhinisha vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini.

    Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe smelitaja jaribio hilo la hivi punde kuwa ni kitendo cha kuudhi.

    Dakika chache baada ya ufyatuzi huo Korea Kusini ilifyatua makombora mawili ya masafa marefu baharini katika hatua ya kuionya Korea Kaskazini kulingana na chombo cha habari cha Yonhap.

    Rais Moon Jae-in alifanya kikao cha dharura na kuonya kwamba kombora hilo litasababisha vikwazo zaidi dhidi ya Korea kaskazini.

    Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa jaribio hilo la hivi karibuni ,likiwa la kwanza tangu vikwazo dhidi ya Korea kaskazini kuimarishwa wiki iliopita lilifanyika katika eneo la Sunan Kaskazini mwa Pyongyang.

    Wakati huo huo Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw Shi Zhongjun mjini Vienna kwenye mkutano wa baraza la Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA, alisema China inapinga kithabiti jaribio la nyuklia lililofanywa na Korea Kaskazini tarehe 3 mwezi huu.

    Amesema China inaitaka Korea Kaskazini izingatie matakwa ya jumuiya ya kimataifa kwenye suala la kuondoa silaha za nyuklia katika Peninsula ya Korea, kuheshimu maazimio ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kusimamisha vitendo vya kuharibu hali ya usalama visivyolingana na maslahi ya nchi, na kutatua suala hilo kwa njia ya mazungumzo.

    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako