Mgogoro wasababisha watu zaidi ya 600 kukimbia makazi yao nchini Ethiopia
Mgogoro uliotokea mwezi huu katika eneo la mpakani kati ya majimbo ya Oromia na Somali umesababisha vifo vya watu kadhaa na watu zaidi ya 600 kukimbia makazi yao.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya habari ya serikali ya Ethiopia haikuweka wazi idadi ya watu waliouawa, bali imesema wengi ni wakulima na wafugaji wa huko.
Hivi sasa serikali ya Ethiopia inashirikiana na maofisa wa serikali za majimbo hayo na vikosi vya usalama kurejesha amani katika eneo hilo mapema iwezavyo.
Chanzo cha mgogoro huo ni tofauti ya maoni kuhusu mgawanyo wa ardhi kwenye eneo la mpakani la majimbo ambao umedumu kwa miaka 20.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |