Hamas yajiandaa kurejesha mazungumzo na Fatah
Kundi la kiislamu Hamas la Palestina limetangaza kuwa linajiandaa kurejesha mazungumzo kati yake na kundi la Fatah.
Mkuu wa kundi la Hamas Bw. Ismail Haniyeh amesema hayo baada ya kumaliza mazungumzo ya siku 11 na maofisa wa usalama wa Misri kuhusu maafikiano ya ndani ya Palestina.
Kwa mujibu wa Bw. Haniyeh, wakati wa mazungumzo hayo ujumbe wake wa ngazi ya juu ulijadili kuhusu hali ya kisiasa na usalama, sera zinazohusu Jerusalem na uhusiano kati ya Palestina na Misri. Amesema kundi la Hamas limekuwa likifanya juhudi kubwa kukomesha mateso kwa watu wa ukanda wa Gaza kwa kutafuta upatanishi na umoja wa kitaifa. Ameliomba kundi la Fatah pia lichukue hatua ikiwa ni pamoja na kuondoa hatua zote zisizofaa dhidi ya Gaza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |