• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (16 Septemba-22 Septemba)

    (GMT+08:00) 2017-09-22 17:35:24

    Mahakama ya upeo Kenya yatoa umamuzi wa kina kuhusu kutupiliwa mbali kwa matokeo ya uchaguzi

    Mahakama ya upeo nchini Kenya imetaja uchakachuaji wa kimakusudi wa data na hatua ya tume ya uchaguzi nchini humo IEBC kukataa kukubali kuwa waliharibu utangazaji wa matokeo kupitia teknolojia kuwa mojawepo wa sababu za kufuta matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8.

    Majaji wakisoma uamuzi wa kina Jumatano kwenye mahakama hiyo aidha

    wamesema matokeo kutoka baadhi ya vituo vya kupigia kura yalikuwa

    hayajatangazwa wakati rais Uhuru Kenyatta alipotangazwa mshindi rasmi wa

    uchaguzi huo.

    Miongoni mwa sababu nyingine zinazotajwa kwenye uamuzi huo wa kina ni

    kwamba tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC haikuhakiki matokeo ya uchaguzi yaliopeperusha kielektoniki kabla ya kutangazwa kwenye kituo kikuu.

    Rais wa mahakama hiyo ya upeo David Maraga anasema uchaguzi sio hafla tu mbali ni mchakato wote kuanzia kupiga kura kutua matokeo na kuyatangaza rasmi na iwapo hatua moja ya kisheria itakiukwa basi hiyo itakuwa hiyo inaathiri mchakato wenywe.

    Lakini huku mahakama hiyo ikitoa uamuzi wake wa kina, chama tawala cha

    jubilee kimeendelea kulalamika kwamba bado kuna dosari nyingi katika uamuzi huo huku kikitaka kura zihesabiwe upya.

    Siku moja kabla ya kutoklewa kwa uamuzi huu wafuasi wa chama hicho walifanya maandamano katika mji mkuu Nairobi na maeneo mengine wakimtaka jaji mkuu na majaji wengine wawili wajiuzulu kwa madai kwamba wanapendelea upinzani.

    Hata hivyo Jaji mkuu David Maraga amewataka wanasiasa kukoma kuishambulia mahakama hiyo na majaji wake na iwapo hawaitaki basi wabadilishe katiba ili kuiondoa.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako