• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (30 Oktoba-3 Novemba)

    (GMT+08:00) 2017-11-03 20:58:19

    Wauguzi wa Kenya wamaliza mgomo uliodumu miezi 5

    Wauguzi wa Kenya wamemaliza mgomo uliodumu kwa miezi 5 baada ya kufikia makubaliano na baraza la magavana la nchi hiyo, CoG.

    Katibu mkuu wa jumuiya ya wauguzi wa Kenya Bw Seth Panyako amesema makubaliano hayo yatatekelezwa kikamilifu ndani ya siku 30 na kuwataka wauguzi warudi kazini kuanzia leo.

    Amesema wafanyakazi wa afya wataongezewa marupurupu yao. Pande mbili pia zimekubaliana kuwa kesi zote zinazohusiana na mgomo huo kwenye mahakamani zitafutwa.

    Wauguzi wa Kenya walianza mgomo mwezi Juni na kusababisha kusitishwa kwa huduma za afya nchini humo, huku wagonjwa wakilazimika kwenda hospitali binafsi.

    Kulingana na makubaliano wauguzi hao wataanza kupokea marupurupu ya kuwa hatarini ya kati ya ksh.20,000 na ksh.25,000 za Kenya kulingana na kundi la kazi alioajiriwa katika kipindi cha bajeti ijayo.

    Mwenyekiti wa magavana nchini Kenya Josphat Nanok amesema kuwa makubaliano hayo na wauguzi yaliafikiwa baada ya majadiliano makali

    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako