Kikosi cha Somalia chavikomboa vijiji kutoka kwa kundi la Al-Shabaab
Kikosi cha usalama cha Somalia kimevikomboa vijiji kadhaa kutoka kwenye udhibiti wa kundi la Al-Shabaab, kusini mwa nchi hiyo.
Ofisa wa kaunti ya Lower Shabelle Bw. Abdifitah Haji Abdulle, amesema kikosi hicho kimetwaa udhibiti wa vijiji vya Mukay Dumis, Digta Gosarow na Idow Gudow katika kaunti hiyo ambapo hakukuwa na upinzani kwa kuwa kundi la Al-Shabaab limeondoka kwenye eneo hilo.
Habari zinasema operesheni hiyo ilipangwa kwenye mkutano wa usalama ulioongozwa na rais Mohamed Abdullahi Mohamed, ambaye ameandaa mpango wa kuongeza nguvu kutoka nchi jirani kusaidia kupambana na kundi la Al-Shabaab.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |