Russia yasema uchunguzi kuhusu matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria si wa kitaalamu
Russia imesema imekubali wiki hii kuendelea na uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria kama sifa ya kundi la wataalamu itainuliwa kwa kiasi kikubwa.
Mkurugenzi wa idara ya udhibiti wa silaha katika wizara ya mambo ya nje ya Russia Bw. Mikhail Ulyanov, amesema Russia inatarajia kuendelea na uchunguzi kwa sababu matumizi ya silaha za kemikali hayakubaliki kwake, na kwa nchi nyingine wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Amesema kundi la wataalamu la pamoja la Shirika linalopiga marufuku silaha za kemikali OPCW na Umoja wa Mataifa lililoundwa kuchunguza mashambulizi ya kikemikali nchini Syria, linapaswa kufanya kazi kihalisi, na sio kazi linayofanya sasa. Ameongeza kuwa baadaye Russia itawasilisha pendekezo lake la utatuzi kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kuongeza muda wa kundi la wataalamu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |