Aliyekuwa mkuu wa jeshi la Sudan Kusini aunda kundi jipya la waasi
Aliyekuwa mkuu wa jeshi la Sudan Kusini Bw. Paul Malong ameunda kundi jipya lenye silaha, akiapa kutwaa nchi na kurejesha amani na utaratibu.
Amesema kundi lake liitwalo "South Sudan-United Front SS-UF" litaongoza nchi hiyo kuelekea kwenye demokrasia na maendeleo zikiwa ni msingi wa kujenga taifa. Amemlaumu Rais Kiir kufanya nchi kuwa ya kifisadi na kufanya maisha ya wananchi yawe magumu.
Bw. Malong alichukuliwa kuwa mshirika mkubwa wa rais Salva Kiir baada ya kushawishi kikosi kimoja cha kikabila kupambana kwa ajili ya serikali ya Rais Kiir.
Lakini Bw. Malong aliondolewa madarakani mwezi Mei mwaka jana, na kuwekwa kwenye kizuizi cha nyumbani kabla ya kuruhusiwa kuondoka nchini mwezi Novemba kwa ajili ya kupata matibabu nchini Kenya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |