Zimbabwe yazialika nchi zaidi ya 40 kushuhudia uchaguzi mkuu
Serikali ya Zimbabwe imezialika nchi 46 ikiwa ni pamoja na China kushuhudia uchaguzi wake mkuu utakaofanyika katikati ya mwaka huu.
Kwa mujibu wa orodha ya nchi na jumuiya zilizoalikwa kushuhudia uchaguzi huo, pia kuna jumuiya 15 za kikanda na kimataifa, zikiwa ni pamoja na Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya COMESA, Bunge la Afrika, na jumuiya ya nchi za Africa Caribbean na Pacific.
Nchi nyingine ni pamoja na Canada, Australia, New Zealand, Japan, Cuba na India.
Kutoka Marekani walioalikwa ni pamoja na seneta wa jimbo la Arizona Bw. Jeffrey Flake ambaye ni msanifu wa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya serikali ya Zimbabwe, na pia ni mjumbe wa kamati ya mambo ya nje ya bunge la Marekani.
Rais Emmerson Mnangagwa amesema uchaguzi mkuu wa Zimbabwe utakuwa huru na wa haki.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |