Spika wa bunge la Somalia ajiuzulu kutokana na mgogoro wa kisiasa
Spika wa bunge la Somalia Mohamed Osman Jawari amejiuzulu baada ya zaidi ya mwezi mmoja wa mvutano wa kisiasa na upande unaompendelea waziri mkuu wa nchi hiyo, Hassan Ali Khaire.
Bw. Jawari ambaye pia ni mbunge wa kuchaguliwa, alikuwa akikabiliwa na hoja ya kutokuwa na imani naye iliyowasilishwa na wabunge kutoka upande wa Waziri Mkuu. Naibu Spika Abdiweli Mudey ameitisha kikao cha bunge hii leo ili kujadili hoja ya kumwondoa spika, siku moja baada ya spika huyo kufanya mkutano wa ndani na rais Mohamed Abdulahi Mohamed wa Somalia.
Wabunge wanamtuhumu Jawari kwa kutumia vibaya madaraka yake na kuzuia marekebisho ya katiba.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |