Macron ahitimisha ziara Marekani
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amehitimisha ziara yake ya kwanza ya kiserikali nchini Marekani Jumatano wiki hii akihutubia mkutano wa pamoja wa Bunge la Marekani na mkutano na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Georgetown.
Wakati wa ziara hiyo ya siku tatu, Macron na Rais wa Marekani Donald Trump walizungumzia ushirikiano wa kibiashara, mazingira, Iran na Syria.
Viongozi hao wawili walikuwepa kuzungumzia tofauti zao na kusisitiza mahusiano ya karibu yaliyoko kati ya nchi hizo na urafiki wao binafsi.
Wakati wakionyesha urafiki wao kwa maneno na vitendo, Trump na Macron wamekiri kuwa wanashirikiana kuondoa tofauti zao katika mambo kama vile mabadiliko ya hali ya hewa na makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa na Iran.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |