Iran yatishia kujitoa kwenye mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia
Katibu Mkuu wa baraza kuu la usalama wa taifa la Iran Bw. Ali Shamkhani amesema, nchi hiyo huenda itajitoa kwenye Mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia kama maslahi yake yatatishiwa.
Bw. Shamkhani amesema, kwa mjibu wa vifungu husika vya Mkataba huo, kama nchi mwanachama anaona hanufaiki na Mkataba huo, anaweza kujitoa. Pia amesisitza tena kuwa Iran ina uwezo wa kuanzisha tena miradi ya nyuklia inayozuiwa na makubaliano ya nyuklia ya Iran.
Mwaka 2015 Iran na pande husika za suala la nyuklia la Iran zilifikia makubaliano, ambapo Iran ilikubali kuzuia mpango wake wa nyuklia na kukaguliwa na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, huku jumuiya ya kimataifa ikikubali kuondoa vikwazo dhidi ya Iran.
Lakini rais Donald Trump wa Marekani amekosoa makubaliano hayo na kutaka Umoja wa Ulaya na bunge la Marekani kuyafanyia marekebisho.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |