Rais wa Sudan Kusini amekataa wito wa upinzani wa kuachia madaraka
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amekataa madai ya makundi kadhaa ya upinzani kuwa anapaswa kuachia madaraka, kama sehemu ya masharti ya awali ya kumaliza zaidi ya miaka minne ya vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Akizungumza katika msiba wa mkuu wa majeshi Jenerali James Ajongo aliyefariki wiki iliyopita nchini Misri, rais Kiir amesema watu wanaopambana na serikali wana masharti yasiyo na maana ili kuleta amani.
Mapema mwezi huu, makundi manane ya upinzani ambayo ni sehemu ya majadiliano ya amani ya Sudan Kusini yalimtaka rais Kiir kujiuzulu wadhifa wake, ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya amani.
Pia makundi hayo yamemtaka rais huyo na aliyekuwa makamu wake Riek Machar kutohusishwa katika serikali ya umoja itakayoundwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |