• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 2-Juni 8)

    (GMT+08:00) 2018-06-08 20:39:54

    Wavuvi wa Tanzania wakamatwa nchini Kenya

    Jeshi la wanamaji wa Kenya liliwakamata raia 109 wa Tanzania kwa kushiriki katika uvuvi haramu katika himaya ya maji ya Kenya katika bahari hindi.

    Wavuvi hao walikamatwa katika eneo la Shimoni , linalomiliki bandari kusini mashariki mwa Kenya karibu na mpaka na taifa la Tanzania na kuwasilishwa mbele ya mahakama ya kaunti ya Kwale siku ya Jumatatu.

    Wavuvi hao walizuiliwa baada ya kushindwa kulipa dhamana ya shilingi 20,000 za Kenya kila mmoja wao lilisema gazeti la Biashara nchini Kenya Business Daily , likimnukuu naibu wa kamishna wa Lungalunga Josphat Biwott.

    Hatahivyo serikali ya Tanzania tayari imeanza harakati za kuhakikisha kuwa raia hao wanaachiliwa huru.

    Naibu waziri wa uvuvi na ufugaji nchini Tanzania Abdalla Ulega ameliambia gazeti la The Citizen nchini humo kwamba juhudi zimeanza ili kuona kuwa tatizo hilo limetatuliwa.

    Ulega amesema tayari wamezungumza na wizara ya maswala ya kigeni na jeshi la polisi ili kuona vile tatizo hilo litakavyoshughulikiwa. Walikamatawa kulingana na sheria za Kenya. Kenya na Tanzania zimekuwa katika msururu wa mgogoro wa kibiashara ambao umekuwa ukizua uhasama katika ya mataifa hayo jirani.

    Mapema mwaka huu mataifa hayo mawili yalianza zoezi la kuweka alama katika mpaka wake kupitia kuondoa vigingi vilivyooza na kuweka vipya.

    Mpaka wa Kenya na Tanzania una urefu wa kilomita 769 na hutumiwa na jamii kutoka mataifa pande zote mbili za mpaka kufanya biashara, kilimo na ufugaji hususan miongoni mwa kabila la Wamasai.

    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako