Chama cha soka cha vunjiliwa mbali nchini Ghana kufuatia tuhuma za ufisadi
Ghana ilivunjilia mbali chama cha soka baada ya rais wake kunaswa katika video akionekana akipokea 'zawadi ya pesa'.
Kwesi Nyantakyi alipigwa picha akipokea dola 65,000 kutoka kwa mwandishi habari mpekuzi aliyejifanya kuwa mfanyibiashara aliye na hamu kubwa kuwekeza katika soka Ghana.
Mpaka sasa hajasema chochote kuhusu tuhuma hizo.
Waandishi wanasema uchunguzi huo uliofanywa na mwandishi habari anayekumbwa na mzozo Anas Aremayaw Anas umezusha maswali kuhusu soka barani Afrika. Serikali ya Ghana imesema hatua za muda za kuongoza soka Ghana zitatangazwa hivi karibuni, kukisubiriwa kuundwa chama kipya. Nyantakyi ni makamu wa rais wa shirikisho la kandanda Afrika na pia mwanachama katika baraza la Fifa - taasisi inayosimamia soka duniani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |