• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 2-Juni 8)

    (GMT+08:00) 2018-06-08 20:39:54

    Mvutano kati ya ras wa Marekani Donald Trump na wenzake wa G7 kuhusu hatua ya marekani kuongeza ushuru kwa bidhaa zinazotoka nchini humo

    Kumekuwa na maneno makali kutoka kwa Rais Donald Trump kuelekea mkutano wa mataifa tajiri G7 unaotarajiwa kufanyika nchini Canada, kwamba inatoza ushuru mkubwa kwa bidhaa zitokazo Marekani na kusabisha mazingira magumu yasiyoenda na sera za kifedha.

    Kitendo cha Trump kuongeza ushuru katika bidhaa za chuma kumemuweka katika mazingira ya kutofautiana na mataifa wanachama wa G7.

    waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau pamoja na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wameahidi kutumia mkutano wa G7 kumshawishi rais Trump dhidi ya msimamo wake kibiashara.

    Macron amesema hatua hatua alizochukua Trump hazina manufaa hata kwa uchumi wa taifa lake. Ameongeza kuwa huwezi kuanzisha vita vya kibiashara na washirika wako.

    Amesema nchi hizo zote zimekuwa zikishirikiana katika mzozo wa Syria na Iraq na maeneo mengine duniani.Hatua ya hivi karibuni ya Rais Trump ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za washirika wake imezua mzozo mpya wa kibiashara.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako