Takriban watu 15 wamefariki alhamisi wiki hii katika moto mkubwa uliokumba soko moja nguo katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.
Zaidi ya watu 70 walijeruhiwa katika moto huo uliotokea katikati ya usiku na kusababisha uharibifu wa mali nyingi.
Soko hilo la Gikomba ndio soko kubwa zaidi katika mji huo na moto hutokea mara kwa mara.
Hatahivyo chanzo cha moto huo bado hakijulikani.
Baadhi ya waathiriwa walichomwa huku wengine wakivuta moshi wenye sumu walipojaribu kuokoa mali yao.
Maafisa wa hospitalini wanasema kulikuwa na watoto watano miongoni mwa waliofariki.
Waliojeruhiwa walikimbizwa katika hospitali tofauti mjini humo.
Soko hilo ni maarufu sana kwa uuzaji wa nguo za mitumba , viatu na mboga, na pia lina maeneo ya kuweka mbao ambayo yaliharibika katika moto huo.
Soko hilo ni maarufu kwa uuuzaji wa nguo za mitumba viatu na hata mboga, na kuna maeneo ya kuuzia mbao ambayo yameharibiwa kupita kiasi katika moto huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |