Watu 83 wajeruhiwa kwenye mlipuko Ethiopia
Mlipuko mkubwa umetokea katika mkutano wa waziri mkuu mpya wa Ethiopia, Abiy Ahmed.
Inaarifiwa kwamba watu 83 wamejeruhiwa huku 6 wakiwa katika hali mahututi.
Imebidi kiongozi huyo mkuu aondoshwe kwa haraka muda mfupi baada ya kutoa hotuba yake wakati mlipuko huo unaodhaniwa kuwa wa guruneti, ulipotokea.
Maelfu walikuwa wamekusanyika katika bustani kuu ya Meskel mjini Addis Ababa katika mkutano ulioandaliwa kuiunga mkono serikali yake Abiy.
Hali ya utulivu sasa imerejea na duru za polisi zinasema wanachunguza tukio hilo.
Abiy aliichukua nafasi ya waziri mkuu Ethiopia baada ya kiongozi aliyekuwepo Hailemariam Desalegn aliopjiuzulu ghafla mnamo Februari huku kukiwa na hali ya hatari na mgogoro wa kisiasa
Shirika la uratibu wa mambo ya kibinadamu la Umoja wa mataifa OCHA limesema inaaminika kuwa waethiopia karibu milioni moja wamekimbia makazi yao kutokana na kuongezeka kwa vurugu za kikabila tangu mwezi Juni mwaka huu.
OCHA imesema takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa watu laki 7.9 katika eneo la Gedeo, na wengine laki 1.8 katika eneo la Guji Magharibi wamekimbia makazi yao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |