Moto mkubwa uliozuka na kuunguza msitu nchini Ugiriki umeua watu 60, huku mamlaka nchini humo zikisema kuwa zinahitaji msaada wa kimataifa ili kukabiliana na moto huo ulio janga baya kuwahi kushuhudiwa kwa zaidi ya muongo mmoja.
Moto mkali unaoshambaa kutokana na upepo mkali umesababisha uharibifu mkubwa katika kijiji kilichoko ufukweni mwa bahari Mati, na kuyaharibi magari na nyumba katika eneo hilo.
Waokozi wameyapata miili ya watu 26 na watoto ambao wanaonekana kukumbatiana walipokuwa wanafariki, wakiwa wamekwama katika moto huo uliozuka mita chache chache kutoka baharini.
Mamia ya wafanyakazi wa vikosi vya zima moto, wanaendelea na jitihada za kuuzima moto huo, huku watu wakiwa wameyakimbia makazi yao katika maeneo ya karibu na mji mkuu wa taifa hilo Athens.
Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras amelazimika kukatisha ziara yake ya Bosnia ili kusaidia uratibu wa hali hiyo,ambayo vikozi vya uokoaji vinasema ni mbaya kuwahi kutokea.
Msemaji wa serikali Dimitris Tzanakopoulos amethibisha kuwa watu 20 wamekufa kutokana na moto huo, amefafanua kuwa wale waliokwama upande wa baharini takribani kilomita 40 kaskazini mashariki mwa mji wa Athens ndiyo waliokufa wakiwa nyumbani kwao na wengine kwenye magari.
Watu 104 wamejeruhiwa kati yao 11 wakiwa katika hali mbaya, lakini watoto 16 nao wamejeruhiwa.
Nchi za Italia, Ujerumani, Poland na Ufaransa wametuma misaada ya ndege, magari na watalaamu wazima moto.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |