Makundi hasimu Sudan Kusini yaafiki kugawana madaraka
Makundi hasimu nchini Sudan Kusini yamesaini makubaliano ya kugawana madaraka mjini Khartoum.
Makubaliano hayo yaliyosomwa na waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bw Al-Dirdiri Mohamed Ahmed, yamesema Salva Kiir ataendelea kuwa rais wa Sudan Kusini katika kipindi cha mpito, huku kiongozi wa upinzani Riek Machar akishika wadhifa wa makamu wa kwanza wa rais.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, makamu wanne wa rais watatoka vyama vinne tofauti. Baraza la mawaziri la mpito litaundwa na mawaziri 35 wanaotoka serikali na upinzani, ikiwa ni pamoja na mawaziri 20 kutoka serikali ya Sudan Kusini, na mawaziri tisa wanaotoka kundi la upinzani SPLM-IO linaloongozwa na Bw. Machar.
Aidha, bunge la mpito litaundwa na wajumbe 550, ikiwa ni pamoja na watu 332 kutoka serikali ya Sudan Kusini, na 128 kutoka kundi la upinzani SPLM-IO.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |