Raia waanza kuchukua fomu za uchaguzi DRC
Mchakato wa kuchukuwa fomu za uchaguzi wa rais na ule wa wabunge wa kitaifa nchini DRC ulianza Jumatano wiki hii kote nchini humo. Tayari baadhi ya wanasiasa wameonyesha nia yao ya kuwania katika uchaguzi wa Desemba 23.
Fomu za kuwania urais zinapelekwa katika Ofisi ya mapokezi ya kutathmini mgombea wa urais katika makao makuu ya Tume ya Uchaguzi CENI jijini Kinshasa.
Wagombea ambao wanatimiza masharti ya kuwania nafasi hizo, wamepewa siku 15 kuwa wamekamilisha zoezi hilo huku sheria ikieleza kuwa atayeruhusiwa kugombea lazima awe raia wa nchi hiyo.
Wagombea wamepewa muda hadi Agsti 8 wawe wamejaza fomu zao. Lakini orodha kamili ya wagombea itajulikana katikati ya mwezi Septemba.
Tayari baadhi ya wanasiasa wametangaza nia ya ya kuwania katika uchaguzi huo, wakati ambapo wengine, kama vile rais anayemaliza muda wake, bado hajatoa msimamo wake wa kuwania au la.
Makamu wa rais wa zamani Jean-Pierre Bemba na Moise Katumbi Chapwe, mshirika wa zamani wa karibu wa rais Joseph Kabila, wameshatangaza nia yao ya kuwania katika uchaguzi huo, na tayari wameahidi kuejea nchini kutoka mmwanzoni mwa mwezi Agosti.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |