Keshi ya Naibu jaji mkuu wa Kenya yasimamishwa
Mahakama Kuu Kenya imesimamisha uendeshaji wa kesi ya ufisadi dhidi ya Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu.
Mwilu amewasilisha ombi katika mahakam hiyo akiomba asijibu mashtaka ya ulaghai, utumiaji mbaya wa mamlaka na kukwepa kulipa kodi, kesi iliyowasilishwa dhidi yake hapo jana na mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma.
Wiki hii bibi Philomena Mwilu alikamatwa kwenye ofisi ya mahakama kuu na makachero kutoka Kurugenzi ya upelelezi wa makosa ya jinai, kwa tuhuma za kuhusika na miamala inayohusiana na kuanguka kwa benki ya Imperial.
Mkurugenzi wa idara ya mwendesha mashtaka ya Kenya Bw. Noordin Haji amewaambia wanahabari kuwa Bibi Mwilu amepelekwa kwenye ofisi za makao makuu ya Kurugenzi ya upelelezi wa makosa ya jinai, kuhojiwa kuhusiana na matumizi mabaya ya madaraka yake na kupokea rushwa.
Hata baada ya mahakama kusimamisha keshi hiyo Haji amesema kuna ushahidi wa kutosha wa kumfikisha mahakamani, na kufanya hivyo ni kwa ajili ya maslahi ya umma.
Kupitia wakili wake, Okongo Omogeni, Mwilu ameambia Mahakama Kuu kwamba kesi hiyo iliyowasilishwa dhidi yake ina hila na ni njama dhidi yake.
Katika ombi lake mahakamani, alikuwa amewashtaki mkurugenzi wa mashtaka ya umma, Idara ya Uchunguzi wa Jinai, Mwanasheria Mkuu na Hakimu Mkuu anayeangazia kesi za ufisadi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |