Rais wa Zimbabwe aunda tume kuchunguza vurugu zilizotokea kwenye uchaguzi mkuu wa Zimbabwe
Rais Emerson Mnangagwa wa Zimbabwe ametangaza kuunda tume ya watu saba kuchunguza vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, na kusababisha vifo vya watu sita.
Tume hiyo itakayoundwa na wenyeji, watu kutoka kanda hiyo na nje ya kanda hiyo, itakuwa chini ya uenyekiti wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Bw Kgalema Motlanthe, na inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake miezi mitatu baada ya kuapishwa kwa Rais Mnangangwa.
Walioko kwenye tume hiyo ni pamoja na Rodney Dickson kutoka Uingereza, aliyekuwa katibu mkuu wa jumuiya ya madola Bw Emeka Anyaoku kutoka Nigeria, na aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange.
Bw. Mnangagwa amesema amesikitishwa na vifo hivyo na kukilaumu chama cha upinzani cha MDC kwa vurugu hizo, na waangalizi wa uchaguzi wamelilaumu jeshi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |