Urusi kufanya mazoezi makubwa ya kijeshi
Urusi inapanga kufanya mazoezi makubwa ya kijeshi yatakayowajumuisha wanajeshi 300,000 mwezi ujao, yakiwa ndio mazoezi makubwa zaidi ya kijeshi tangu vimalizike vita baridi.
Waziri wa ulinzi Sergei Shoigu alisema vikosi kutoka China na Mongolia vitashiriki kwenye mazoezi hayo maeneo ya kati kati na mashariki mwa Urusi.
Aliyafananisha mazoezi hayo ya kijeshi kwa jina "Vostok-2018" na yale ya kisovieti ya mwaka 1981 ambayo yalihusisha pia mazoezi ya kuishambulia Nato.
Mazoezi hayo yanakuja wakati kuna msukosuko kati ya Nato na Urusi.
Bw Shoigu alisema vifaru 36,000 na magari mengine ya kijeshi yatashiriki kwenye mazoezi ya Vostok-2018, kuanzia Septemba 11 hadi 15 pamoja na ndege 1,000. Vostoik ni neno la kirusi linalofahamika "mashariki".
Akitaja mazoezi ya kisovieti ya mwaka 1981, alisema: "Kwa njia fulani yatafanana na ya Zapad-81, lakani pia kwa njia fulani yanaweza kuwa makubwa."
Kiwango cha mazoezi ya Vostok-2018 ni sawa ni kile kilitumwa kwenda vita vikuu vya pili vya dunia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |