Rais Emmerson Mnangagwa wiki hii ameiapisha tume ya kimataifa ya kuchunguza chanzo cha vurugu zilizotokea Agosti Mosi baada ya uchaguzi mkuu wa Zimbabwe.
Tume hiyo itaongozwa na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Bw. Kgalema Motlanthe, na itakuwa na wajumbe kutoka Uingereza, Nigeria, Tanzania na wenyeji wawili.
Watu sita waliuawa baada ya wanajeshi kuwafyatulia risasi waandamaji wa upinzani waliozusha vurugu kwenye maandamano ya kulalamikia tume ya uchaguzi kuchelewa kutangaza matokeo ya uchaguzi.
Pamoja na mambo mengine, tume hiyo itachunguza wahusika na viongozi wao, malengo yao na mbinu zao kwenye maandamano, na mazingira yaliyofanya jeshi kushiriki, na kiasi cha nguvu iliyotumika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |