Sudan Kusini yakabiliwa na changamoto katika kutekeleza mpango mpya wa amani
Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia operesheni ya ulinzi wa amani Bw. Jean-Pierre Lacroix amesema kuwa, pande za Sudan Kusini zinakabiliwa na changamoto katika kutekeleza makubaliano mapya ya amani.
Bw. Lacroix amesema makubaliano hayo yaliyosainiwa na rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na kiongozi wa kundi la wapiganaji Bw. Riek Machar ni hatua umuhimu kwani yanaweka mwongozo wa amani kupitia mageuzi, mabadiliko ya kisiasa, usalama, maendeleo ya kijamii na ya kiuchumi, pamoja na upatanishi wa taifa.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia uratibu wa mambo ya kibinadamu UNOCHA imesema kuwa, matukio 78 ya kibinadamu yalitokea mwezi Agosti nchini Sudan Kusini, mengi kati yao yalitokea mjini Jonglei, Equatoria ya kati na Upper Nile.
Asilimia 23 ya matukio hayo yalihusisha unyanyasaji dhidi ya wafanyakazi wa mambo ya kibinadamu huku asilimia 26 yakihusisha vurugu dhidi ya vitu vya kibinadamu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |