Jeshi la Burkina Faso laharibu vituo kadhaa vya makundi ya kigaidi
Jeshi la Burkina Faso limetoa taarifa kuwa jeshi la anga la nchi hiyo limefanya operesheni dhidi ya vituo vya makundi ya kigaidi vilivyoko mashariki mwa nchi hiyo.
Taarifa imesema, baada ya kupata habari za kuaminika, jeshi hilo lilituma ndege za kivita kusaka na kuharibu vituo vya makundi ya kigaidi mashariki mwa nchi hiyo.
Magenge mawili ya watu wenye silaha wasiojulikana Septemba 15 walishambulia kwa nyakati tofauti vijiji viwili na kusababisha vifo vya watu wanane.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |