Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inatishia kuichukulia hatua za Kimataifa nchi ya Angola, kufuatia hatua ya Angola kuwafukuza raia wake wanaokadiriwa kuwa 200,000 kwa madai kuwa walikuwa ni wahamiaji haramu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC Leonard She Okitundu amesema, Kinshasa inaitaka Luanda kuchunguza kwa kina aliyeamuru kufukuzwa kwa raia wake na kuchukuliwa hatua, la sivyo itachukua hatua zaidi, kauli aliyoitoa huku akishtumu hatua hiyo.
Serikali ya Angola kwa upande wake imekuwa ikikanusha kuwa iliwafukuza wakimbizi hao kwa lazima kutoka katika mkoa wa Lunda Norte.
Hivi karibuni Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa-UNHCR lilisema lina wasiwasi mkubwa kutokana na wimbi kubwa la idadi ya wakimbizi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC wanaorejea nyumbani kufuatia hatua ya serikali ya Angola kufukuza wahamiaji.
Raia hao wa DRC walikuwa wakifanya kazi katika machimbo ya madini yasiyo rasmi huko Kaskazini Mashariki mwa Angola, kabla ya kufurushwa na kwamba siku ya Jumatatuwiki Oktoba 15 ilikuwa ni siku ya mwisho ya wageni kupaswa kuondoka nchini humo.
Zaidi ya raia 200,000 wa DRC walikimbilia nchini Angola kwa sababu za kiusalama.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |