Rais wa Kenya kuhudhuria maonesho ya uagizaji wa bidhaa ya China
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ataongoza ujumbe mkubwa wa wakulima na wafanyabiashara wa maua kwenye maonyesho ya uagizaji wa bidhaa ya China yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mjini Shanghai.
Ikulu ya Kenya imetangaza kuwa kwenye maonyesho hayo yatakayofanyika kuanzia tarehe 5 hadi 10 ya mwezi ujao, makubaliano mbalimbali yatasainiwa.
Taarifa iliyotolewa na ikulu hiyo imesema baadhi ya makubaliano yatakayosainiwa yatafungua fursa kwa asilimia 40 ya bidhaa freshi za kilimo kutoka Kenya, kama maparachichi, embe, stevia na korosho kuingia kwenye soko la China.
Taarifa pia imesema Rais wa Kenya anatarajiwa kusaini makubaliano ya kuanzisha kikundi cha mazungumzo ya biashara, kujadili ushuru unaotozwa kwa chai na kahawa kutoka Kenya, na kutafuta fursa nyingine za soko kwa bidhaa za Kenya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |