Waziri mkuu wa Ethiopia alaani maandamano ya askari wenye silaha kuwa yamekiuka katiba
Waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed amelaani maandamano ya askari wenye silaha wa Ethiopia kuwa yamekwenda kinyume na katiba, ambayo yanalenga kuzuia mageuzi yanayoendelea.
Askari 250 wa Jeshi la ulinzi la Ethiopia walifanya maandamano mjini Addis Ababa wakilalamikia mishahara na marupurupu madogo, na kuzingiria jumba la taifa na ofisi ya waziri mkuu.
Maandamano hayo pia yamesababisha mgongano kati ya askari hao na walinzi wa waziri mkuu, baada ya walinzi wa Ofisi ya waziri wa Ethiopia kuwazuia kuingia kuonana na Bw. Ahmed wakiwa na silaha.
Hali hiyo ilizua hali ya hatari na kusababisha barabara kufungwa katika eneo hilo huku mtandao ukizimwa kwa saa kadhaa.
Lakini bwana Abiy alitumia njia ya kuwafayisha mazoezi polisi hao na kuleta msisimko.
Akizungumza na wabunge siku ya Alhamisi , bwana Abiy alisema kuwa bila amri ya kufanya press ups swala lote zima lingeongezeka na kuzua wasiwasi mkubwa.
Tangu achukue mamlaka mnamo mwezi Aprili , bwana Abiy amefanya mabadiliko -ikiwemo kuwaachilia huru maelfu ya wafungwa wa kisiasa , kutopiga marufuku makundi yaliopigwa marufuku na kuleta amani kati yake na taifa la Eritrea.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |