Pande husika za mapigano ya Yemen zatarajiwa kufanya mazungumzo ya amani mwanzoni mwa Desemba huko Sweden
Waziri wa ulinzi wa Marekani Bw. James Mattis amesema, pande husika zinazopingana nchini Yemen zinatarajiwa kufanya mazungumzo ya amani mwanzoni mwa Desemba huko Sweden, ili kujadili namna ya kumaliza mapigano ya hivi sasa haraka iwezekanavyo.
Bw. Mattis amesema, serikali ya Yemen na kundi la Houthi zitaweza kushiriki kwenye mazungumzo hayo, na kwamba ili kumaliza mapigano hayo na kutatua mgogoro wa kibinadamu nchini Yemen, Saudi Arabia pia inatakiwa kushiriki kwenye mazungumzo hayo. Hivi sasa Saudia na Falme za Kiarabu (UAE) zimesimamisha operesheni za kijeshi karibu na mji wa bandari wa Hudaydah nchini Yemen, lakini mapigano yanaendelea.
Takwimu zilizotolewa na shirika lisilo la kiserikali Save the Children zimeonyesha kuwa, watoto elfu 85 walio na umri wa chini ya miaka mitano huenda wamefariki kutokana na utapiamlo tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vitokee nchini Yemen.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |