Waziri mkuu wa Israel atakuwa waziri wa ulinzi wa nchi hiyo
Waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanjahu ametangaza kuwa atakuwa waziri wa ulinzi wa nchi hiyo.
Bw. Netanjahu amesema hayo kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika makao makuu ya wizara ya ulinzi mjini Tel Aviv-Yafo, ameongeza kuwa hali ya usalama ya sasa ya Israel imekuwa ngumu na nyeti, hivyo haina haja ya kufanya uchaguzi wa kabla.
Bw. Netanjahu amesema kuwa kufanya uchaguzi mapema kuliko mpango uliowekwa ni jambo la kutowajibika, anajitahidi kutatua mgogoro uliokabiliwa na serikali ya muungano, ili kuepuka kufanya uchaguzi mapema.
Hadi sasa Bw. Netanjahu amekuwa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel, waziri wa elimu ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Jewish Home Bw. Naftali Bennett anataka Netanjahu kumteua kuwa waziri wa ulinzi, ama sivyo, vyama vya viti 8 vya bunge vilivyoongozwa naye vitaondoka kutoka kwa serikali ya muungano.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |