Uingereza yamteua waziri mpya wa kushughulika masuala ya Brexit
Serikali ya Uingereza imemteua Stephen Barclay kuwa waziri anayeshughulika masuala ya Brexit Umoja wa Ulaya na kuchukua nafasi ya Dominic Raab aliyejiuzulu tarehe 15 mwezi huu.
Ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza imetoa taarifa kuwa waziri Barclay atafanya maandazili kwa mujibu wa hali mbili ya kujitoa kwenye umoja huo kukiwa na makubaliano na bila ya makubaliano.
Waziri Barclay ana msimamo thabiti kuhusu kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya, na aliwahi kufanya kazi katika wizara ya afya na bima ya umma ya Uingereza.
Siku moja kabla, serikali ya Uingereza ilimteua Amber Rudd kuwa waziri wa ajira na pensheni, na kuchukua nafasi ya Esther Mcvey.
Mapema mwezi Mei Baraza la Mawaziri nchini Uingereza lilidhinisha rasimu ya mswada wa makubaliano juu ya nchi hiyo kujiondoa katika Umoja wa Ulaya maarufu kama Brexit.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |