Vikosi vya Somalia na AMISOM kufanya operesheni ya pamoja kuwatimua wapiganaji wa Al -Shabaab
Vikosi vya tume ya umoja wa Afrika AMISOM na Somalia vinapanga kufanya operesheni ya pamoja katika eneo la Jubba ya kati, kusini mwa Somalia, ili kuwafurusha wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab.
Naibu mkuu wa operesheni wa AMISOM Bw. Charles Tai Gituai amesema operesheni ya pamoja itahusisha vikosi vya AMISOM, Serikali ya jimbo la Jubbaland na vikosi vya jeshi la taifa.
Bw. Gituai pia alifanya mazungumzo na makamanda wa vikosi mbalimbali vya AMISOM vilivyoko katika jimbo la Jubbaland, na kuvipongeza kwa kazi yao nzuri iliyochangia kuwepo kwa amani kiasi katika jimbo la Jubbaland.
Naibu Rais wa Jubabaland Bw Monamud Sayid Aden, amesema maandalizi kwa ajili ya operesheni ya pamoja yamefikia kwenye hatua nzuri, na ziara iliyofanywa na Bw. Gutuai ina lengo la kufanya uratibu wa vikosi vya AMISOM, Jubbaland na jeshi la taifa ili viweze kufanya operesheni ya pamoja.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |