Ethiopia yaanza kuaondoa wanajeshi wake kwenye mpaka na Eritrea
Ethiopia imethibitisha kuwa imeanza kuwaondoa wanajeshi wake kwenye mpaka wenye utata na jirani yake nchi ya Eritrea kama sehemu ya utekelezaji wa makubaliano yaliyotiwa saini baina ya nchi hizo mwezi Julai mwaka huu.
Makubaliano haya yalimaliza miongo miwili ya mzozo wa kimipaka ulioshuhudia maelfu ya raia wakipoteza maisha.
Kuondolewa kwa wanajeshi wa Ethiopia kwenye mpaka huo limekuwa ndio takwa kubwa la utawala wa Asmara.
Nchi hizi mbili zilipigana vita kati ya mwaka 1998 na 2000 ambapo licha ya kufikiwa kwa makubaliano ya amani miaka miwili baadae, uhusiano baina ya nchi hizi mbili ulikuwa wa utata mkubwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |