Makubaliano ya kusitisha vita yatekelezwa Hodeidah, Yemen
Serikali ya Yemen na kundi la upinzani la Houthi wamefikia makubaliano ya kusimamisha vita katika mazungumzo ya amani yaliyoongozwa na Umoja wa Mataifa nchini Sweden.
Kamati ya uratibu ya RCC imesema, inatarajia kuyatekeleza kwa haraka makubaliano hayo katika mji wa Hodeidah unaodhibitiwa na kundi la Houthi.
Msemaji wa kundi hilo Bw. Mohammed Abdul-Salam amesisitiza nia ya kundi hilo kutekeleza makubaliano ya Stockholm, na kusimamisha vita mjini Hodeidah.
Kwa upande wake, serikali ya Yemen pia imetoa amri kwa makamanda wa kamandi ya nne ya kikanda na vikosi viliyoko katika mji huo kusimamisha vita kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |