Duru mpya ya Mazungumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani yafunguliwa Washington
China na Marekani wiki hii zimefanya duru mpya ya mazungumzo ya ngazi ya juu ili kutatua mgongano wa kiuchumi na kibishara kati ya nchi hizo mbili.
Mazungumzo hayo yanaashiria kuwa mafanikio yamepatikana kutokana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Marekani Donald Trump mjini Buenos Aires, Argentina mwezi uliopita.
Viongozi wa nchi mbili wanaona pande zote mbili zinapaswa kufikia makubaliano ya kunufaishana ndani ya siku 90, ili kumaliza mgongano wa kibiashara wa kutozana ushuru mkubwa kwenye sekta ya uagizaji kutoka nje, ambayo yameendelea kwa miezi mingi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |